Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Ahmad Khatami, usiku wa jana katika hafla ya kumuenzi Kiongozi Shahidi, Ayatullah al-Udhma Imam Khamenei (ra), iliyoandaliwa na taasisi kuu za Hawza katika ukumbi wa Imam Khomeini (ra) ndani ya Haram Tukufu ya Bibi Fatimah Maasumah (as), huku akirejelea hafla za kuwaenzi na mazishi ya viongozi wakubwa wa kidini kama Imam Khomeini (ra), Shahidi Ayatullah Raisi na Shahidi Haj Qassem Soleimani, alisema: "Tulishuhudia mazishi makubwa zaidi katika historia, ambayo yalikuwa ni mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Iran, jambo ambalo hata vyombo vya habari vya kigeni vililikiri."
Mjumbe wa Ulamaa wa Baraza la Kulinda Katiba aliongeza kuwa; kumwamini Mwenyezi Mungu ilikuwa miongoni mwa sifa kuu za Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, na kwamba alikuwa na imani ya dhati katika ahadi za kweli za Mwenyezi Mungu, ikiwemo ushindi na msaada wa haki dhidi ya batili. Alisema siri ya mapenzi na umaarufu mkubwa aliokuwa nao Imam Shahidi miongoni mwa wananchi ilikuwa ni imani hiyo.
Mjumbe wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum, huku akisisitiza kwamba kulipiza kisasi na kudai damu ya Imam Shahidi ni matakwa ya Umma wa Kiislamu, amesema: "Moja ya ujumbe muhimu zaidi uliojidhihirisha katika mazishi ya Kiongozi Shahidi ni dai la pamoja la Umma wa Kiislamu la kutaka kulipiza kisasi na kuwawajibisha waliohusika na jinai hii."
Ayatullah Khatami amesisitiza kuwa kupandishwa kwa bendera nyekundu na kaulimbiu zilizopazwa na wananchi kumeonesha wazi kwamba damu ya Kiongozi Shahidi haitasahaulika kamwe, na kwamba taifa la Iran linaendelea kulifuatilia dai hilo kwa umakini na uzito mkubwa.
Maoni yako